Kitumbua Kimeingia Mchanga
by Assorted
Sold out
KES 493
Kitumbua Kimeingia Mchanga ni tamthilia inayozusha mawazo kuhusu tofauti zilizoko baina ya mila na tamaduni za kale na za kisasa kuhusu suala la ndoa. Pia imeshughulikia uhuru wa vijana wa kileo kinyume na matakwa ya wazee wao. Fikirini hakubali kuchaguliwa mke na babake, Bw Mambo na nyanyake, Bi Hoja. Wazee wake wanaona jambo la kumchagulia mtoto wao mke ni jukumu lao. Vilevile, wanamtuhumu Hidaya, msichana ambaye Fikirini anataka kumuoa, kuwa ni kiruka njia, mhuni na muovu. Je, Fikirini atashinda kuwatoa shaka na kuwashawishi wazee wake wamkubalie analolipenda? Je, ndoa ya Fikirini itafanikiwa?
Said A. Mohammed alizaliwa Unguja tarehe 12.12.1947. Alipata digrii yake ya B.A. Education (1979) na ya M.A. Isimu (1981) katika Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam; na shahada ya Udaktari (Ph.D: 1985) huko Leipzig, Ujerumani. Ni mwalimu aliyefundisha shule za sekondari, chuo cha ualimi, taasisi na vyuo vikuu nchini Kenya, Japani na sasa ni Profesa katika Chuo Kikuu cha Bayreuth, Ujerumani. Ni mwandishi maarufu wa fasihi ya Kiswahili. Vitabu vyake vilivyochapishwa na Oxford University Press ni pamoja na Kivuli Kinaishi na Kiza katika Nuru.
UPC | 50SRB20564 |
---|---|
SKU | 50SRB20564 |
Any item you order from our site, we will deliver to you, or for you, anywhere in Kenya.
We deliver for free for all orders above Ksh 2,000 and charge a standard fee of Ksh 250 for all orders below Ksh 2,000.
Delivery takes place within 72 hours after order confirmation.
This product does not have any reviews yet.
Add your review