Mfalme Edipode
by Assorted
KES 395
KES 534
Mchezo huu ni tafsiri ya mmojawapo wa michezo ya misiba iliyo mashuhuri iliyotungwa na yule mwandishi wa Kigiriki, Sofokile, kiasi cha miaka 420 kabla ya Kristo. Unatuwekea mbele yetu hadithi nzuri mno ya mfalme ambaye, pamoja na kuwa na moyo laini, ana ndweo ya kiburi cha kuzawa nacho. Kiburi hicho ndicho kinachompeleka kwenye kifo kiovu baada ya kumuua babake na kumuoa mamake bila ya kujua.
Katika tafsiri hii iliyofanywa kutokana na nakala kadha wa kadha za Kiingereza, Samuel Mushi ameuhifadhi ule moyo na tabia ya ushairi asilia wa Kigiriki na papo hapo akashikamana na mwendo wa ushairi wa Kiswahili kwa kadri inavyowezekana. Katika utangulizi wake anakokoteza kwamba ingawa mchezo huu ulitungwa kwa mujibu wa utamaduni wa Kigiriki wa kale, wahusika wake na hisia zao ni za kiulimwengu mzima na, kwa hivyo, mchezo wenyewe unaweza kuchezwa katika mazingira ya Kiafrika.
Samuel Mushi, mfasiri wa mchezo huu, alikuwa mwalimu wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alielimishwa katika vyuo vikuu vya Makerere, Berkeley na Yale, na alipata kuwa Mkuzaji wa Lugha na Tungo za Kiswahili katika Wizara ya Maendeleo na Utamaduni, Tanzania, toka Machi 1965 hadi Juni 1967.
UPC | 50SRB20569 |
---|---|
SKU | 50SRB20569 |
Any item you order from our site, we will deliver to you, or for you, anywhere in Kenya.
We deliver for free for all orders above Ksh 2,000 and charge a standard fee of Ksh 250 for all orders below Ksh 2,000.
Delivery takes place within 72 hours after order confirmation.